FURSA
YA BIASHARA NI NINI?

Baada ya
hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan). Kwa hiyo unapofikiria ni
biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo
husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli
nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya
biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana
nazo, baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji ni kama:
1.
Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi?
2. Je unapotaka
kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi?
3. Je
unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko
vipi?
4.
Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya
kutosha?
5. Vitu
gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila
siku? 6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani?


Vile vile
tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi
zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya
Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa
na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza
kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi
kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao
n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa
kuyatatua.
Nawatakia
kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii
inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje;
yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki
n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika
hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi.
Source: http://gshayo.blogspot.com
No comments:
Post a Comment