MAKALA YA LEO NITAKUFUNDISHA
JINSI YA KUTENGENEZA WEBSITE YAKO PAMOJA NA BLOG YAKO KWA MUDA MCHACHE TU
Kila mtanzania ana ndoto ya kuwa
na maisha mazuri ila wengi wetu tuna shindwa kutoka kimaisha kwasababu tu
hatuzijui fursa zetu ,kuna niia mbali mbali wewe kama kijana unaweza kujiajili
na kujikimu kimaisha ,
Unaweza kuanzisha blog yako inayo
weza kukutengenezea pesa kwa namna moja ama nyingine yote haya utajifunza hapa
hapa katika Makala zetu za technologia hii mpyaa
Unaweza kutengeneza pesa kwa
kuanzisha blog yako kwa kuweka matangazo ya watu pia wewe kama ni mfanya
biashara unaweza ukaitangaza biashara yako duniani kote kwa kupitia blog yako
hivo basi Tuangalie namna ya kuanzaa blog yako.
Hapa ndio mahali husika katika
kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama
ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao.
Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
NJIA YA KWANZA
BLOGGER Kupitia uwanja huo au platform hiyo
inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na
jina ulipendalo wewe mfano:- http://jinalablog.blogspot.com,
hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka
jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako
Bofya hapa ili kutengeneza blog yako Create
a new Blog
NJIA YA PILI
WORDPRESS Hapa pia utaratibu ni kama hapo
mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo
(features) vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na
uwanja au platform ya wordpress. Namna ya jina la blog yako itakuwa katika
mfano huu:- http://jinalabloglog.wordpress.com.
Ukitaka kuwa na blog kupitia wordpress tafadhali bofya hapa, Sign up For New Wordpress
Naamini hadi sasa umeisha elewa
namna ya kuweza kuanzisha blog yako, wakati mwingine nitazungumzia jinsi ya
kuweza kuwa na blog yako ikiwa na domain yako mwenyewe mf:- www.domainyako.com. Endelea kusoma Makala zetu ili upate kujua
mengi Zaidi na uweze kujua namna mbali mbali ambavo watu wana wini kimaisha.
IFANYE BLOG YAKO KUWA NA MUONEKANO MZURI ZAIDI
Kuna
njia nyingi sana za kufanya blog yako iwe na muonekano wa kipekee na wenye
mvuto kwa kila atakae ingia katika blog yako nitakufundisha chache na rahisi
ili upate kuelewa upesi na kuifanyia kazi blog yako kuanzia sasa
HTML ni aina ya lugha inayo tumika
kuaandaa web pages kwa kutumia hii hapa itaweza kutengeneza pages za blog yako
katika muonekano utakao upenda wewe ,mara nyingi ili kuifanya page yako
ipendeze kwa marembo ya aina mbali mbali itakulazimu pia utumie lugha ina itwa CSS.ni ligha inayo weza kuifanya page yako ikae
katika muundo wowote upendao
Vile vile HTML inasimama
badala ya Hyper Text Markup Language. pia HTML ina maana zifuatazo
HTML is a markup language
A markup language is a set
of markup tags
The tags describe document
content HTML
Documents contain HTML tags
and plain text
HTML documents are also called web pages
Katika HTML
kuna kitu kinajulikana kwa jina la HTML Tags, je nini maana yake? Na
hutumiwaje? Unapotumia html lazima utumie hiki kitu kwani bila ya Html tag
huwezi kufanya lolote kwani ndio ufunguo wa lugha hii ya kutengenezea website.
Html Tag inakuwa katika mfano kama huu ikiwa na maana kuwa ufungo wa neno
unakuwa katikati ya mabano hayo yenye pembe (angle brackets). HTML Tags huwa
mara nyingi huja kwa jozi, yaani kama kuna <html>basi lazima kuwe kuna</html>
ikiwa na maana kwamba, ile ya kwanza ni ya kufungua na ya pili ni ya kufunga.
Ila kumbuka
kuwa tag ya mwisho ambayo ndiyo ya kufunga huwa inafanana na ile ya kufungua
isipokuwa tu hii ya kufunga lazima ianze na alama ya mkwaju "/” kabla ya
kumalizia neno husika. Mfano <mfano>……………</mfano> na huwezi kukuta
kitu kama hiki <mfano>……..</body>
HTML ELEMENT
Hii ni kila
kilichopo baina ya tag mbili pamoja na tag zenyewe. Mfano <p>this is my
first page</p> Hivyo basi, ukikutana na sentensi kama hiyo <p>this
is my first page </p>basi ujue kuwa hiyo ni HTML Element.
Kumbuka kuwa kazi ya tag ni kuamrisha
yale maneno yaliyo baina ya tag hizo mbili, kuwa kwa jinsi tag hizo
zilivyohitaji. Nitakupa mfano lakini sio katika HTML ila nimetumia mbinu hii
ili kukuelewesha. Tuchukulie mfano unataka maandishi yako yatembee, maandishi
yenyewe labda ni haya "WEBSITE NZURI” na katika ujuzi wako ukaona kuwa tag
inayofaa kuamrisha maandishi yatembee inaitwa <marquee>, hivyo basi
katika kutengeneza kwako utaandika kama ifuatavyo: <marquee>WEBSITE
NZURI</marquee>
Kuna program zinazotumika kuandikia tag zetu ili tuweze
kutengeneza website kama vile,
Adobe
Dreamweaver
Microsoft
Expression
Web CoffeeCup
HTML Editor
Lakini kwa
kujifunza HTML nasisitiza sana kutumia Notepad na ni njia rahisi na bora sana
katika kujifunzia kuliko kwenda mbali huko. Nadhani kila mtu anajua kuwa katika
Windows kuna program ndogo inayoitwa notepad, program hii kazi yake sana utaona
ni kuandikia maneno lakini ina umuhimu mkubwa sana kwani hutumika kutengeneza
baadhi ya application ndogo ndogo za kompyuta. Hivyo kwa hii hii tutaitumia
katika kutengeneza web page.
Kwa asiyejua
kuifungua hii fuata maelekezo haya:
To start
Notepad go to: Start All Programs, Accessories,kisha bofya notepad
itafunguka. Muonekano wake ni kama huu hapa chini: Sasa hapo ndipo tunapoandika
HTML Tags ili kufanikisha utengenezaji wa web page. Ni kama ndoto kwani hakuna
lolote litakalowekwa humo ndani isipokuwa ni maandishi tu, lakini itatokea
kurasa nzuri kabisa ya tovuti.
Notepad |
Adobe Dreamweaver |
Ungana nami tena kwa makala zinazo endelea pia kama una maswali au
maoni tafadhali walisiliana nami kupitia
pia +255765327325
+255766518985
No comments:
Post a Comment