Mgombea Urais kupitia CCM Dr.John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa
mji wa Lamadi kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao
kuwa akiingia madarakani atahakikisha wananchi hao wanaondokana na tatizo sugu
la upatikanaji maji.
Mgombea Ubunge jimbo la Busega Dk. Raphael chegeni akihutubia wakazi wa
mji wa maji kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizoongozwa na mgombea urais wa
CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani (kushoto) ,wakipena mikono na Mgombea ubunge wa
jimbo la Busega kupitia CCM Dk. Raphael Chegeni wakati wa mkutano wa kampeni za
kumnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika mji wa
Lamadi wilaya ya Busega mkoani Simiyu
Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Simiyu Dk. Titus Kamani akiteta jambo na mgombea wa Urais kupitia CCM
Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano na wakazi wa mji wa Lamadi, Busega.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi
Sapiwi wakati akiwa njiani kuelekea Meatu.
Wananchi wa Bariadi wakishangilia kwenye mkutano wa mgombea wa Urais
kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli
Mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa
Maetu kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa
atatatua tatizo kubwa la maji kwa kuchukua maji kutoka ziwa Victoria.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mr. Blue akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Meatu.
Wasanii wa Original Komedi wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM
uliofanyika viwanja vya stendi Meatu.
Mbunge wa jimbo la Kisesa Ndugu Mhaga Mpina akihutubia wakazi wa kisesa
kwenye mkutano uliofanyika Mwandora ambapo aliwataka wananchi hao
kumpigia kura mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani ni
kiongozi muadilifu na mpenda maendeleo.
No comments:
Post a Comment