Watu wengi
wanakata tamaa na hali ya unyanyapaa juu ya kilimo,Tunasikia watu wengi hasa wa
mijini wakisema kilimo ni uchafu na ni kwa watu maskini na wasio na elimu hizo
ni Imani potofu zinazo jengwa na watu wachache wasio jua thamani ya kilimo ,
Ebu
fikiria katika hali ya kawaida ni mahitaji mangapi kwa siku unayahitaji katika
kula , pia kama wakulima wangegoma kuleta bidhaa mjini je maisha ya mjini
yangukuwaje ,hapo jibu kila mtu atakuwa analo
Mara
nyingi tumeona hata katika mashindno mbali mbali majaji huwakatisha tamaa
washiriki kwa kuwaambiaa warudi shamba kana kwamba shamba ni jambo la ajabu
sana na ni la aibu
Katika
uhalisia hakuna kitu cha kijanja kama wewe mkulima utajitengenezea kipato chako
tena cha uharari kwa kulima tu ni dhana za watu wachache tu zinazo potosha
kilimo katika taifa hili”
Kilimo
kina thamani na kinaweza kuwa sekta yenye faida kubwa kwa sababu watu wengi
wanahitaji kula , viwanda vingi vinategemea bidhaa toka kwa wakulima ko utaona
uchumi wa nchi unajikita Zaidi katika kilimo sasa kama kilimo kina manufaa yote
hayo kwanini tukipe kisogo
Kila sekta
inalipa kama utajitoa na kufanya kazi kwa bidi na ndivo hata katika kilimo,Kwa
hiyo kijana usiogope jembe kilimo ni fedha na kinaweza kuwa mkombozi wa maisha
yako cha msingi kifanye kuwa ndiyo ajira yako
CHANGAMOTO
MBALI MBALI KATIKA KILIMO
Wakulima
wengi wanakosa maarifa ya kukipelekea kilimo katika hatua nyingine ;wanaridhika
mara tu wanapopata fedha kidogo baada ya mavuno
SULUHISHO
Jinunulie
mbolea yako na si usubiri tu ruzuku za pembejeo
Uliza
katika makundi ya wakulima wengine au bwana/bibi shamba juu ya mazingira yako,
Fahamu
muda mzuri wa kupanda mazao yako ili kuepuka wadudu waaribifu na jinsi ya
kujitengenezea mboji Mazao yanakuwa imara Zaidi na kuhimili mashambulizi ya
wadudu kama utapanda kabla ya kipindi cha unyevu nyevu”
Katika
kundi lako la wakulima wanachama wanaweza kufata pembejeo wilayani au mikoani
kwa mawakala wa kilimo ,Matunda yanaweza kuonekana mapema
Uhifadhi
wa chakula ni njia nzuri ya kuongeza thamani ya mazao yako,hasa kama unasubiri
hadi bei iongezeke sokoni na hapo utapata bei nzuri
Watu
katika vyama vya wakulima huweza kupata sehemu ya kuhifadhi mazao au mnaweza
kupunguza gharama za kusafirisha mazao kwajili ya kupeleka ghalani
Pia mbinu
Zaidi za kijadi katika kuhifadhi mazao kama vile vihenge hutumika kuokoa jahazi
UHABA WA
MASOKO
Kutafuta
soko la bidhaa zako linaweza kuwa changamoto kubwa sana kwako,yaweza kuwa
umbali kutoka shambani kwako hadi sokoni au wakati mwingine kutopata kile
unacho hitaji
Unaweza
kupanga kabla; jadiliana kuhusu bei na fanya makubaiano ya bei na mteja wako au
dalali kabla ya kuufikisha mzigo
Kuwa na
mkakati mbadala;kama mnunuzi hakubaliani na bei yako peleka biashara yako
sehemu nyingine au tafuta njia nyingine ya kuuza bidhaa zako
Ni
vyema kuanzisha chama ili muweze kujadiliana na kupata bei
nzuri ya pamoja
No comments:
Post a Comment