vodacom

vodacom

movie

Utalii

Tangaza Biashara Yako Nasi..


+255758061575 & umojannguvu@gmail.com

umj

katiba

katiba

bloger

bloger

Blog

Blog

slider1

slider

Taswira za Maendeleo ya ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam Wezesha na MB Mobile! Kilimo ndo Mpango Mzima. Authorities allow railway to pass through national parks & Maendeleo Agricultural Technology Fund Tanesco Na Maendeleo Welcome to Maendeleo Bank PLC

Sunday, September 13, 2015

TUNAELEWA NINI KUHUSU FURSA YA BIASHARA

FURSA YA BIASHARA NI NINI?


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara (mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya. Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara (Business idea) huanza kwanza kwa kuchunguza fursa zilizopo katika eneo husika. 
Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan). Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo, baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji ni kama: 
1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi? 

2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi? 

3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko vipi? 

4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya kutosha? 

5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila siku? 6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani? 
Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza kutokana na mazingira husika. Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika jamii kuwa ni kawaida, 
kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida, lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza wazo la biashara. Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo. 
Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua. 
Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi. 
Source: http://gshayo.blogspot.com

Je unaweza kujiajili kwa computer yako ya nyumbani

  
Jibu ni ndio , kwanini tunasema ndio basi ungana nami katika Makala hii niliyo kuandalia siku ya leo ili utambue fursa yako ni ipi ukiwa na computer yako ya nyumbani .
Vijana wengi wanapo kuwa na computer zao wanaishia kusikiliza music, Kuangalia videos pamoja na kucheza games tu hawatambui kwamba kupitia computer yako ya nyumbani unaweza ukatengeneza pasa pasipo kuwa na kipato chochote.
Nitakudokeza njia mbalimbali wewe kijana kama mwanafunzi au kijana wa nyumbani tu, Kwa leo nitakudokeza jinsi ya kutengeneza pesa kwa ku tengeneza kalenda yenye muonekano mzuri na tofauti tofauti unao weza kumfanya kila mtamazaji apende kuitazama na hata kuinunua 
Kutengeneza kalenda hakuitaji elimu kubwa sana wala kipato kikubwa sana ni wewe tu na juhudi zako na kujituma kwako ,Utaweza kuanza kuandaa kalenda yako kwa kutumia program ya Microsoft publisher iliyopo katika package yako ya Microsoft office katika computer yako 
Vile vile unaweza kutumia program kama
Adobe photoshop
Microsoft office
Adobe photoshop itakusaidia katika kuandaa picha na kuziweka katika mitindo mbali mbali
Jinsi ya kufungua Microsoft publisher nenda katika uwanja wako wa start button katika computer yako
Bofya all programs
Bofya katika package yako ya Microsoft office baada ya hapo chagua Microsoft office publisher 
Baada ya kufungua itaonekana kama picha inavo onesha hapo chini
   
Itakuwa rahisi Zaidi kwako kama utatumia Microsoft office 2013 package kwasababu kuna template nzuri na za kisasa 
Baada ya kudisign calender yako utaweza kuweka picha za aina mbali mbali kama picha za familia, za marafiki, makampuni na za shule pia kama uatakuwa umepata oda na mtu basi utaweza kumsikiliza yeye anahitaji picha ya aina gani
   
Utaweza kujifunza Zaidi na Zaidi namna za kufanya ili uweze kutengeneza calender yako basi unaweza kupata mafunzo mbali mbali na hlmservice kuanzia sasa
Kama unahitaji kujua Zaidi unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa mawasiliano yafuatayo 
+255765327325 
henrylameck@gmail.com

ZINGATIA HAYA UNAPO NUNUA COMPUTER

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA LAPTOP.
Kwa Mwanafunzi, Mfanyabiashara, Photographer au videographer. Mcheza Games, Mtumiaji wa Nyumbani /matumizi ya kawaida.
1. Wanafunzi
Mambo makuu kwa mwanafuzi ni bei ya kubebeka kwa laptop yenyewe. Laptop inayoweza kubebeka kutoka darasa mpaka darasa, au darasani mpaka kwa sam muuza chipsi, ndio cha msingi , kwa hiyo kwa wanafunzi wengi huwa ni Netbooks ambazo hazina gharama kubwa, ni ndogo, inatumia nishati ndogo na ni around tshs 450,000-700,000. Ubaya wake ni kwamba hizi huwa na screen ndogo na hutumia single-core CPUs ambazo zimepunguzwa nguvu.

Option nyingine ni laptop yenye inchi 13, nyembamba, ambayo portability yake (uwezo wa kubebeka) ni mzuri, na inapendeza zaidi wa kuandikia au kutumia ukiwa umekaa sehemu tulivu na sio haraka haraka. CPU zake ni dual-core na mara nyingi huja na optical drives. Mfano mzuri ni MacBook za Apple zenye inchi 13.
Nini Cha Kuzingatia: At least 1GB ya RAM; 160GB au zaidi za HDD; inchi 13 au chini ya hapo.
2. Mfanyabiashara
Wale ambao mara nyingi huwa barabarani huitaji mashine iliyo faster, inaydumu na charge na zaidi ya yote
ThinkPad za Levono na Latitude za Dell ni mifano miwili mizuri ya laptop zilizotengenezwa zikimlenga mfanyabiashara (au kwa lugha rahisi, anayesafiri mara kwa mara) . Bidhaa zote mbili zina security nzuri na imara, pia hardware za in-built software zake zinafanya kazi vizuri na OS (Operating System) yoyote e.g windows, Ubuntu, etc (lakini sio Mac, ).Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 160GB au zaidi kwa Hard Disk; 12 mpaka 15-inch display; Windows Vista Professional au Windows 7 Professional; mobile broadband modem.
 
3. Mpigapicha na/au Videographer
Wachezaji wa games sio watu pekee wanaohitaji processor yenye nguvu, graphics za ukweli na hard disk space kuuuubwa. Kwa wale ambao wanatengeneza high-definition video or high-resolution photographs huitaji mashine inayojitosheleza hasa! Nimekuwa mpenzi mkubwa sana wa video producing. Miaka ya nyuma nikaanza kujifunza After Effects, FinalCut, etc. Ila kilichosumbua ilikuwa ni mashine. PC yangu RAM 1GB, hard disk 80 GB na vikolombwezo vingine vya kimaskini.
Nikaishia kwenye Windows Movie Maker 
MacBook Pro inch 15 mpaka 17 zile za Apple ndio maarufu na nzuri kwa kazi hii (expensive though). MacBook ni nzuri pia kwa sababu software ya Final Cut, ambayo ndio maarufu DUNIANI kote kwa video producing, inapatikana kwenye Mac pekee. (Adobe’s Photoshop inapatikana kwenye platform tofauti tofauti, hivyo usijali).
Cha msingi hakikisha SANA SANA SANA kuwa una RAM kubwa…….. 8GB za RAM ndio penyewe. Pia hard disk ya 500GB ingependeza sana, kwa sababu redering in real-time inahitaji RAM/processor faster na inakula space hasa.
Cha kuzingatia: 4GB-8GB of RAM; Hard Disk ya 320GB yenye uwezo wa 7,200rpm, yaani 7,2000r per minute (usijali kama huelewi inamaanisha nini, wewe mwambie muuzaji hivyo ukiwa na uso mkavu..bhaaaas); 17-inch or larger display.
4. Wachezaji Games
Games za sasa hivi zinafika mpaka 20GB na hiyo setup tu! Mambo yanaanza kuwa mengi kama video card, sound drivers, na makolombwezo kibao! Kama wewe ni gamer, basi utahitaji desktop computers, zenye flexible upgradeability, faster components, na yenye uwezo wa kupoa haraka.Ila kwa siku za hivi karibuni, laptops zinazowafaa gamers zina-hit sana.
Ningependekeza kuanzia Core 2 Quad za Intel na Core i7 CPUs kwa 3D gaming, kwa sababu zina GPU nzuri ,kama GeForce N260 za Nvidia.
Ya kuzingatia: 4GB mpaka 8GB za RAM; 320GB au zaidi kwa Hard Disk; display ya inchi 17 au zaidi; bila kusahau the most important, discrete graphics GPU.
5. Mtumiaji wa Nyumbani
Mtu yoyote ambaye hayupo kwenye vipengele nilivyovitaja hapo juu anafiti hapa.Mtumiaji huyu huitaji desktop machine ambazo sio movable,Mashine hizi hutengenezwa kwa asili ya kukaa sehemu moja, ile jikoni, sebuleni, chumbani, etc.
Zile laptop za inchi 15 bado ni maarufu ingawa zile za inchi 14 na 16 zinakuja juu siku hizi. Kila mtengenezaji wa PC hutofautiana na mwingine na huzidiana kila mmoja katika sehemu tofauti. Usikimbilie kununua mashine kubwa na kutumia hela nyingi.
Ya kuzingatia: 2GB mpaka 4GB za RAM; 250GB au zaidi kwenye Hard Disk; Display ya inchi 14-16; DVD burning optical drive (kwa asili ya ku-burn CD).
hayo ndio ya kuzingatia uendapo kukunua PC. Kuwa makini na kujua ni kundi lipi size yako.
Kwa maelezo Zaidi wasiliana kwa     +255765327325
                                                     henrylameck@gmail.com

TENGENEZA BLOG YAKO KWA MDA MFUPI TU UONE MAFANIKIO



MAKALA YA LEO NITAKUFUNDISHA JINSI YA KUTENGENEZA WEBSITE YAKO PAMOJA NA BLOG YAKO KWA MUDA MCHACHE TU
Kila mtanzania ana ndoto ya kuwa na maisha mazuri ila wengi wetu tuna shindwa kutoka kimaisha kwasababu tu hatuzijui fursa zetu ,kuna niia mbali mbali wewe kama kijana unaweza kujiajili na kujikimu kimaisha ,
Unaweza kuanzisha blog yako inayo weza kukutengenezea pesa kwa namna moja ama nyingine yote haya utajifunza hapa hapa katika Makala zetu za technologia hii mpyaa 
Unaweza kutengeneza pesa kwa kuanzisha blog yako kwa kuweka matangazo ya watu pia wewe kama ni mfanya biashara unaweza ukaitangaza biashara yako duniani kote kwa kupitia blog yako hivo basi Tuangalie namna ya kuanzaa blog yako.


Hapa ndio mahali husika katika kujifunza namna ya kuwa na blog yako na kuifanya iwe na mafanikio makubwa kama ambavyo wengine wamefanikiwa kupitia blog zao.

Kuna namna mbali mbali za kuwa na blog ila leo hapa nitazungumzia mbili tu ambazo ni rahisi sana. Kumbuka kuwa kuwa na blog yako mwenyewe hakuna gharama yoyote zaidi ya muda wako na ubunifu wako.
NJIA YA KWANZA
BLOGGER Kupitia uwanja huo au platform hiyo inayomilikiwa na Google unaweza kuanzisha blog yako mwenyewe ambayo itabebwa na jina ulipendalo wewe mfano:- http://jinalablog.blogspot.com, hapo ambapo nimekoleza kwa maandishi ya rangi nyekundu ndipo ambapo utaweka jina la blog yako. Utaratibu mzima utaupata wakati ukiwa unaisajiri blog yako Bofya hapa ili kutengeneza blog yako Create a new Blog 
NJIA YA PILI
WORDPRESS Hapa pia utaratibu ni kama hapo mwanzo ila hizi ni nyanja (Platforms) tofauti na zinatofautiana vikolombwezo (features)  vya uboreshaji wa blogs. Hapa ukianzisha blog yako itabebwa na uwanja au platform ya wordpress. Namna ya jina la blog yako itakuwa katika mfano huu:- http://jinalabloglog.wordpress.com. Ukitaka kuwa na blog kupitia wordpress tafadhali bofya hapa, Sign up For New Wordpress
Naamini hadi sasa umeisha elewa namna ya kuweza kuanzisha blog yako, wakati mwingine nitazungumzia jinsi ya kuweza kuwa na blog yako ikiwa na domain yako mwenyewe mf:- www.domainyako.com. Endelea kusoma Makala zetu ili upate kujua mengi Zaidi na uweze kujua namna mbali mbali ambavo watu wana wini kimaisha.
IFANYE BLOG YAKO KUWA NA MUONEKANO MZURI ZAIDI 
Kuna njia nyingi sana za kufanya blog yako iwe na muonekano wa kipekee na wenye mvuto kwa kila atakae ingia katika blog yako nitakufundisha chache na rahisi ili upate kuelewa upesi na kuifanyia kazi blog yako kuanzia sasa
HTML ni aina ya lugha inayo tumika kuaandaa web pages kwa kutumia hii hapa itaweza kutengeneza pages za blog yako katika muonekano utakao upenda wewe ,mara nyingi ili kuifanya page yako ipendeze kwa marembo ya aina mbali mbali itakulazimu pia utumie lugha ina itwa CSS.ni ligha inayo weza kuifanya page yako ikae katika muundo wowote upendao
Vile vile HTML inasimama badala ya   Hyper Text Markup Language. pia HTML ina maana zifuatazo
HTML is a markup language
A markup language is a set of markup tags
The tags describe document content HTML
Documents contain HTML tags and plain text
HTML documents are also called web pages
Katika HTML kuna kitu kinajulikana kwa jina la HTML Tags, je nini maana yake? Na hutumiwaje? Unapotumia html lazima utumie hiki kitu kwani bila ya Html tag huwezi kufanya lolote kwani ndio ufunguo wa lugha hii ya kutengenezea website. Html Tag inakuwa katika mfano kama huu ikiwa na maana kuwa ufungo wa neno unakuwa katikati ya mabano hayo yenye pembe (angle brackets). HTML Tags huwa mara nyingi huja kwa jozi, yaani kama kuna <html>basi lazima kuwe kuna</html> ikiwa na maana kwamba, ile ya kwanza ni ya kufungua na ya pili ni ya kufunga.
Ila kumbuka kuwa tag ya mwisho ambayo ndiyo ya kufunga huwa inafanana na ile ya kufungua isipokuwa tu hii ya kufunga lazima ianze na alama ya mkwaju "/” kabla ya kumalizia neno husika. Mfano <mfano>……………</mfano> na huwezi kukuta kitu kama hiki <mfano>……..</body>
HTML ELEMENT
Hii ni kila kilichopo baina ya tag mbili pamoja na tag zenyewe. Mfano <p>this is my first page</p> Hivyo basi, ukikutana na sentensi kama hiyo <p>this is my first page </p>basi ujue kuwa hiyo ni HTML Element.
Kumbuka kuwa kazi ya tag ni kuamrisha yale maneno yaliyo baina ya tag hizo mbili, kuwa kwa jinsi tag hizo zilivyohitaji. Nitakupa mfano lakini sio katika HTML ila nimetumia mbinu hii ili kukuelewesha. Tuchukulie mfano unataka maandishi yako yatembee, maandishi yenyewe labda ni haya "WEBSITE NZURI” na katika ujuzi wako ukaona kuwa tag inayofaa kuamrisha maandishi yatembee inaitwa <marquee>, hivyo basi katika kutengeneza kwako utaandika kama ifuatavyo: <marquee>WEBSITE NZURI</marquee>
Kuna program zinazotumika kuandikia tag zetu ili tuweze kutengeneza website kama vile,
Adobe Dreamweaver
Microsoft Expression
Web CoffeeCup HTML Editor
Lakini kwa kujifunza HTML nasisitiza sana kutumia Notepad na ni njia rahisi na bora sana katika kujifunzia kuliko kwenda mbali huko. Nadhani kila mtu anajua kuwa katika Windows kuna program ndogo inayoitwa notepad, program hii kazi yake sana utaona ni kuandikia maneno lakini ina umuhimu mkubwa sana kwani hutumika kutengeneza baadhi ya application ndogo ndogo za kompyuta. Hivyo kwa hii hii tutaitumia katika kutengeneza web page.
Kwa asiyejua kuifungua hii fuata maelekezo haya:
To start Notepad go to: Start All Programs, Accessories,kisha bofya   notepad itafunguka. Muonekano wake ni kama huu hapa chini: Sasa hapo ndipo tunapoandika HTML Tags ili kufanikisha utengenezaji wa web page. Ni kama ndoto kwani hakuna lolote litakalowekwa humo ndani isipokuwa ni maandishi tu, lakini itatokea kurasa nzuri kabisa ya tovuti. 

Notepad
Adobe Dreamweaver


 
Ungana nami tena kwa makala zinazo endelea pia kama una maswali au maoni tafadhali walisiliana nami kupitia 

pia +255765327325
      +255766518985

JE UNATAKA KUJUA JINSI YA KUINSTALL OPERATING SYSTEM UKIWA NYUMBANI

Unaweza kujitengenezea kipato wewe mtanzania kwa kujiajili katika shughuli mbalimbali,Sio lazima uajiliwe katika makampuni makubwa ama serikalini ama mahala popote bali unaweza ukabuni namna yoyote ya kutengeneza kipato na kutimiza ndoto zako, Kwako mwanafunzi unae maliza chuo sasa ama uliepo nyumbani tu una computer yako ila una shindwa utaanza vipi kujikimu kimaisha hii ni fursa yako sasa kujua jinsi ya kuandaa Operating system (OS)  na kufanya installation katika Computer yoyote.
Kuna njia mbali mbali za kuweza kuweka Operating system (OS) katika computer yako leo nitakupa Njia mbili ambazo ni rahisi Zaidi kwako.
Katika njia zote hizo ni kwajili ya Windows 7 zote pamoja na Windows 8 zote 
VIFAA VYA KUWA NAVO KABLA HUJAANZA CHOCHOTE

Kwa njia ya kwanza hakikisha una flash Drive ambayo itakulazimu uifanye kuwa bootable bila ya kufanya hivo itakuwa sio rahisi kukamilisha zoezi lako isipo kuwa kama computer yako itaweza ku boot hivo hivo,Je utaifanya vip Flash yako iweze ku boot
POWER ISO 
Power Iso ni software inayo weza kukusaidia kutengeneza flash iweze ku boot unaweza kupata software hiyo kwa kubofya hapa http://www.poweriso.com/thank-you.htm
Kabla ya kuaandaa flash yako kumbuka window 7 au 8 itakuwa katika muonekano huu




Hakikisha ina kuwa katika mfumo wa image kama picha inavo onesha hapa chini



Baada ya kufungua software ya power Iso copy mafile ya windows na paste katika uwanja wa power iso the uta save file yako as (.Iso) image utakuwa umebadilisha

 ANDAA FLASH IWEZE KU BOOT KATIKA COMPUTER

Fuata hatua zifuazazo

Juu kabisa ya software nenda katika uwanja umeandikwa tools bofya hapo itakuja menu ina vitu vingi  wewe utachagua create bootable Usb Drive itafunguka box hii hapa 
Wakati huo umechomeka flash yako katika Computer hatua inayo fuata ni ku bofya mahali pameandikwa image source file mahali ulipo save image yako ya window itakuletea window zote zilizo katika mfumo wa image kama hivi



Chagua window unayo taka then Bonyeza Start Button Software itafanya kazi yake mpaka mwisho itakuambia ume fanikiwa sasa una weza ukaweka flash katika computer yoyote na kuweka wendow bila shida.

JINSI YA KUINSTALL WINDOW KATIKA COMPUTER YAKO BAADA YA KUANDAA FLASS



Weka Flash yako katika computer alafu zima computer yako baada ya hapo washa ,kabla computer haijawaka press button F12 juu kabisa ya computer yako au minya escape 
Baada ya hapo computer itakudai unataka kuboot toka wapi basi chagua mahali pa usb and flash drive uweze ku boot flash yako. Hapo window itafanya installation hadi mwisho kabisa na hatua zingine ni za kawaida tu kuset password pamoja na kuandika user name ya computer.
JINSI YA KU INSTALL LINUX KATIKA COMPUTER
Kuna software mbali mbali zinazo weza kusaidia kutengeneza flash yako iweze ku boot linux katika flash yako
Unetbootin-windows-585, Ni moja ya software nzuri na rahisi kukusaidia kutengeneza flash yako iweze ku boot linux
Muonekano wake ni kama hivi hapo chini

Ni rahisi kutumia kuliko Power iso lakin hakikisha linux yako iwe katika mfumo wa image

Asante sana ndugu msomaji 

Mimi mwandishi wako henry Lameck unaweza wasiliana nami moja kwa moja katika email yangu hapa chini
 
pia +255765327325
      +255766518985


Ijue tehama awe mkombozi sasa......




 
COMPUTER SERVICES

Karibu tena mtanzania mwenzangu katika tovuti hii mpya ,Utapata habari nyingi zinazo husiana naTechnologia ya sasa.Mimi kama mtanzania mwenzako nimechukua fursa hii kuamasisha watanzania wa leo kutumia zaidi Technologia ya kileo ili kutimiza ndoto zao ,Je Ni vitu gani kuwa navo ili kutimiza ndoto zetu. Pia Kutakuwa na Makala zinazo elezea matumizi mazuri ya computer ,kuteneza home network, bila ya kutumia vifaa vingi na vya gharama,je ni computer gani inafaa kwa matumizi yako,na ipi haifai kwa matumizi yako.Karibu sana wapenzi wasomaji .
SOMA MAKALA MBALIMBALI ZINAZO HUSIANA NA TECHNOLOGIA YA SASA
Moja ya Makala muhimu na watu wengi wanapenda Zaidi ni hasa kujua maisha ya mafanikio yanapatika vipi , je wewe mtanzania wa leo unaitaji kukua kiuchumi . Basi Usikose mada hizi tutakazo kuwa naza katika blog yetu hii Nzuri
kwa leo Nitapenda kukupa Ufahamu Kidogo Kuhusiana na Computer ,

JE COMPUETER NI NINI?


Wewe mtanzania unahitaji kujua computer ni kitu gani kabla ya kuanza kuifanyia kazi pia unabidi kufahamu umuhimu wa kuwa na computer nyumbani kwako ,Leo nitakuwa sijakutendea haki kama sita kufahamisha maana ya computer pamoja na matumizi ya computer ,Kuna maana nyingi sana ya kifaa computer ,utaweza kuelezea maana za computer kutokana na matumizi ya kila siku lakini kwa maana kuu tuta sema kwamba “Computer ni Kifaa kinacho tumia umeme kinacho weza kufanya mambo makuu matatu ambayo ni kuhifadhi data mbali mbali ambazo unaweka ndani ya computer ,Baada ya kuweka data zako katika computer basi zita kuwa processed ndani ya computer na mwisho wa yote tuta pata output ambazo ni matokoe ya data kuwa processed”



Vile vile Computer tutaweza kusema ni kifaa kinacho weza kukurahisishia wewe mtanzania kuingia internet na kufanya shughuli zako mtandaoni mfano mzuri unapo tuma email, unapo chati katika mitandao ya kijamii kama facebook,twiter,nk tutajifunza mengi kuhusu internet endelea kusoma mada hii ili kujua mengi Zaidi ,
Mambo ya msingi kuhusu intaneti 

Wavuti ni nini, na ni jinsi gani unavyoweza kuifanyia kazi?
Unavyochunguza vidokezo juu ya usalama katika Vizuri Kufahamu, unaweza ukawa na maswali kadhaa kuhusu wavuti ni nini na jinsi ya kutumia aina maarufu ya huduma mtandaoni. Tafadhali angalia majibu haya kutoka Googlers na pata maelezo zaidi kuhusu kuingia mtandaoni, kupata maelezo na kuabiri katika mtandao, na kuunganisha na kushiriki mtandaoni.



Kuingia mtandaoni
Intaneti ni nini?

Intaneti ni mtandao wa kompyuta zilizoenea duniani kote zote zikiwa zimeunganishwa moja kwa nyingine. Unapojiunga kwenye Intaneti unakuwa na ufikiaji wa World Wide Web, ambayo ni sawa na maktaba iliyojaa kurasa za maelezo.

Unaunganishwa vipi kwenye Intaneti? Shughuli ya ISP ni ipi?


Kabla hujaanza kuuchunguza mtandao, utahitaji kuweka mpango na ISP. ISP, au Mtoa Huduma za Intaneti, ni kampuni inayokuruhusu kufikia Intaneti na huduma nyingine za mtandao. Wanatoa njia tofauti za kuunganishwa ikiwa ni pamoja na kupiga simu, kebo, fiber optics au Wi-Fi. Muunganisho hizi tofauti huamua kasi ya ufikiaji wako wa mtandao. 
Baada ya kuona maana ya computer na internet basi tuangalie umuhimu wa kuwa na computer ni upi na tutatumia vipi computer kuinua hali zetu za kiuchumi
Computer ina matumizi mengi sana ukiwa nyumbani,kwako mwanafunzi, pia hata maofisini ,pia unaweza ukajiajili kupitia computer yako hapo ulipo
Kwa mwanafunzi utaweza kusomea computer pamoja na kutafuta mengi kwenye internet, kwa mfanya biashara utatunza kumbukumbu zako za kibiasha pia hata za kiofisi
Unaweza kutengeneza pesa kupitia computer yako ya nyumbani kama utakuwa mbunifu wa kujitangaza kupitia computer yako.Blogger ni njia pekee inayo weza kuitangaza biashara yako kwa kasi na kwa watu wengi duniani ,Blog ni mfano wa website ambayo unaweza kuweka matangazo yako ya kibiashara pamoja na kujitangaza wewe ni nani ?
Ni rahisi sana kutengeneza blog yako na kujitangaza Zaidi, pia nitakuelekeza jinsi ya kuanzisha blog yako ya kibiashara pamoja na kupata muonekano mzuri zidi wa blog yako
Mara nyingi unapo tengeneza blog itakulazimu uwe katika internet lakini kuna njia mbali mbali za kutengeneza blog kuonekana katika muonekano mzuri Zaidi kwa kutumia Microsoft word, Microsoft publisher pamoja na Excell, Sio hivo kuna lugha mbali mbali za kutengeneza kurasa za blog yako
Kuna mfano wa lugha ina itwa HTML, CSS, JavaScript ni lugha nzuri za kutengeza kurasa zako za blog yako yote hayo utayapata hapa katika tovuti yetu hii ya hlmservice.
COMPUTER GANI INA FAA KWA MATUMIZI YAKO


Chagua computer inayo weza kukidhi mahitaji yako ukizingatia uwezo wa computer je unahitaji utumie katika matumizi gani, Kwa mfano wewe ni designer na katika designing yako unatumia program kubwa kama adobe photoshop basi chagua computer yenye ukubwa mkubwa kwa kuangalia Hard Disk Isiyo pungua 500Gb na processor 2.20GHz na RAM(Random Access Memory) Sio chini ya 2.0Gb , kwa matumizi ya kawaida kabisa pia fuata vigezo hapo juu lakini itapendeza kama utachukua computer yenye ukubwa wa wastani ili kuifadhi kumbukumbu zako rahisi na kwa wingi Zaidi


Unaweza ukawa na home network nzuri inayo weza kukidhi mahitaji yako kabisa kwa kutumia simu yako ya smart phone, Hapa inakuwa haina haja ya kutumia modem kutengeneza network nyumbani hata oficine ,Kupitia simu yako ya smartphone unaweza kutengeneza wireless inayo weza kumudu kwa computer Zaidi ya tatu hadi nne kikubwa ni kujiunga vifurushi vya internet kama kawaida ya vifurushi vya mitandao yote alafu tengeneza wireless yako ufurahie internet na yenye kasi Zaidi





Jinsi ya kutengeneza wireless kwa kutumia smartphone yako fuata hatua zifuatazo 



Hatua ya kwanza
Ingia Katika sehemu ya setting kwenye simu bofya Mahali pameandikwa More..Utaona  maelezo haya juu kabisa pameandikwa Wireless&Networks chini yake utaona
Airplane Mode
Vpn Settings
Tethering & Portable hotspot
Mobile Networks
Hatua ya pili
Bofya mahali wameandika Tathering & Portable hotspot itakuonesha jinsi ya kuiwasha wireless yako lakini kabla ya yote unahitaji kuitengeneza kwa jina unalo taka kwa kubofya mahali pameandikwa Set-up Wi-Fi hotspot ,Andika jina upendalo pia kuna mahali pa kuweka passwork kama unahitaji kwa jili ya kuzuia watu wengi kutumia wireless yako basi andika passwork na iwe siri kwako tu ,Endapo utasambaza password yako utaona matumizi yako ya bundle ni makubwa kwa sababu utakuwa umeruhusu watu wengi watumie wireless yako
Hizo hatua mbili juu ni kwa wale watu wanao tumia simu za Android lakini kwa wanao tumia windows phone ni rahisi Zaidi kwani utaenda mahali pameandikwa setting halafu Internet sharing,Uta seti password na jina la wireless yako.
Kabla ya kufanya yote hayo hakikisha computer yako ina support wireless kama hapana basi angali kama kuna driver za wireless kama computer itakuwa hai support basi zoezi hili litakuwa gumu kwako.
Asante sana mpenzi msomaji wa Makala yangu hii ya leo mungu akubariki usikose kusoma habari nyingi Zaidi na Zaidi mada zinazo kuja mbele ni nzuri Zaidi tutafundisha jinsi ya kuinstall windows katika computer yako ,jinsi ya kuiandaa flash yako iweze kuboot window moja kwa moja badala ya kutumia CD” Mimi mwandishi wako henry Lameck unaweza wasiliana nami moja kwa moja katika email yangu hapa chini
pia +255765327325
      +255766518985
 
 
perPage: 7,